Na mwandishi wetu;
Mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif, amehudhuria
uzinduzi wa kampeni za chama hicho uliofanyika leo, Agosti 28, 2025, katika
viwanja vya Tanganyika Packers, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo umefanyika sambamba na kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi kwa vyama vyote vya siasa, kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).
Tarehe hii inaashiria mwanzo rasmi wa harakati za kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Dkt. Jafari ni miongoni mwa wagombea walioteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika majimbo mbalimbali nchini, yeye akiwakilisha Jimbo la Busanda lililopo Wilaya ya Geita mkoani Geita.
Uzinduzi huo umeonesha nguvu ya CCM katika maandalizi ya uchaguzi, na umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama, wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge, pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.
0 Comments