Na nwandishi wetu;
Wananchi wa Kata ya Nyaruyeye wakisikiliza kwa makini sera za Mgombea Ubunge Jimbo la Busanda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
wa kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, Dkt. Jafari amesisitiza mambo manne ya
kipaumbele atakayoyashughulikia mara moja ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa
eneo hilo.
Ujenzi wa barabara ya lami ya Geita–Kahama, ambayo ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa wakazi wa eneo hilo. Kuboresha huduma za maji safi na salama kwa wakazi wa Nyaruyeye ili kupunguza adha ya kutafuta maji.
Mgombea Ubunge Jimbo la Busanda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif akihutubia wananchi wa kata ya Nyaruyeye.
Sambamba na hayo Dkt. Jafari amesema atahakikisha upatikanaji wa mikopo kwa
vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, ili kuwawezesha kiuchumi na kupambana
na umasikini.
Amesema katika uongozi wake atashirikiana vyema na serikali za mitaa
na wadau mbalimbali kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi.
Wananchi wa Kata ya Nyaruyeye wakipunga mikono juu kama ishara ya kukubaliana na hotuba nzuri ya Mgombea Ubunge Jimbo la Busanda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif.
Dkt. Jafari ameweka dhamira yake ya ndani kuwa atakuwa
karibu na wananchi wake, kusikiliza kero zao na kuhakikisha Jimbo la Busanda
linapiga hatua katika sekta mbalimbali hasa maendeleo.
"Hatutaki maneno, tunataka vitendo. Barabara, maji na mikopo kwa makundi maalum ni vitu vitatu vya haraka tutakavyovifanyia kazi. Nawahakikishia ushirikiano wa karibu katika kila hatua ya maendeleo," amesisitiza Dkt. Jafari.





0 Comments