Na mwandishi wetu;
Mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif, amewahakikishia wananchi wa Kata ya Busanda kuwa atatoa msukumo mkubwa katika ajenda za halmashauri, hasa kwenye uboreshaji wa barabara ya Katoro–Busanda–Nyakamwaga.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni
uliofanyika katika kata hiyo, Dkt. Jafari amesema kuwa anafahamu changamoto
kubwa inayowakabili wananchi kutokana na hali ya barabara hiyo, na kwamba baada
ya kuchaguliwa atahakikisha inaboreshwa ili ipitike kipindi chote cha mwaka.
"Nafahamu kuwa barabara
yenu ina changamoto. Nitakwenda kusukuma kwa nguvu zaidi ili TANROADS
waichukue. Ikishapanda TANROADS, itafanyiwa matengenezo mara mbili kwa mwaka na
hivyo itapitika muda wote," amesema Dkt. Jafari.
Wananchi wamempongeza mgombea huyo
kwa kujitokeza kueleza mipango yake waziwazi, wakisema kuwa barabara hiyo ni
kiungo muhimu kwa usafirishaji wa mazao na shughuli za kila siku.




0 Comments