Na Editha Edward;
Akizindua mradi huo kiongonzi wa mbio za
mwenge kitaifa mwaka 2025 ameipongeza Ruwasa kwa kukamilisha mradi huo kwa
ufasaha huku akiwataka wananchi kuiunga mkono serikali kwa kulinda miundo mbinu
ya maji.
Mradi huo wa maji umegharimu zaidi ya milioni mia nne na ulianza kutekelezwa mwaka 2021 na kukamilika mwezi juni 2023 na unatoa huduma ya maji kwa wananchi.
Mradi huo umepunguza muda uliokuwa
unatumika kufuata maji mbali ambapo sasa muda huo unatumika kufanya shughuli
nyingine za uzalishaji na maendeleo kwa jamii.
Mradi huo umefungua frusa za kiuchumi ikiwemo uendeshaji wa viwanda vidogo vidogo vya kusafisha dhahabu, kufyatua tofari, bustani za miti na mbogamboga na umepunguza magojwa yanayotokana na ukosefu wa maji safi na salama.
0 Comments