Na Editha Edward;
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru
kitaifa Ismail Ali Ussi amempongeza mwekezaji mzawa aliejenga kituo cha Afya
kilichopo kata ya Bukandwe wilayani mbogwe ili kuwahudumia wakazi wa maeneo
hayo.
Amesema hayo mara baada ya kuweka
jiwe la msingi katika kituo hicho cha Afya ambapo amesema kuwa nchi hii
inajengwa na watanzania wenyewe na wilaya ya mbogwe inajengwa na wanambogwe
wenyewe hivyo wawekezaji wazawa wanao wekeza katika nchi yao wanafanya vyema
ili kuwahudumia watanzania wenzao.
Ussi amesema kuwa ameisaidia serikali,
kwa waliosoma udaktari, fani ya uhudumu, mapokezi kwa wanaoishi mkoa wa
Geita kupata ajira kwani hakuna
mwajiliwa mgeni, wote ni wazawa hivyo vijana wetu wamepata kazi katika kituo
hicho cha afya.
Akisoma taarifa mkurungenzi wa kituo
cha Afya Gakala Bunga Dadu amesema kuwa mradi huo unathamani ya shiringi
bilion tatu.
Dadu amesema kuwa lengo la
mradi nikusaidia wananchi wa kata ya Bukadwe pamoja na kata jirani kupata
huduma bora za afya na kibigwa
0 Comments