Na Editha Edward;
Mwenge
wa Uhuru, umeridhishwa na ujenzi wa mradi wa visima vitano vya maji vilivyopo
Wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ali Ussi, amesema hayo baada ya kukagua mradi huo na kuridhishwa na utekelezaji wake.
Amewataka
wananchi kushirikiana na viongozi katika kulinda miundombinu ya maji ili iweze
kuduma kwa muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Grace Kingalame, ametumia fursa hiyo kwa kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika wilaya hiyo.
Kwa
upande wake, Kaimu Meneja wa RUWASA Mhandisi Suzana Gogadi, amesema vijiji
vitano vinanufaika na mradi huo wa maji na kwamba unagharimu zaidi ya milioni
miatatu.
Mwenge
wa Uhuru ukiwa wilaya ya Nyang'hwale utatembelea na kukagua kisha kuweka mawe
ya msingi katika miradi 11 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5
0 Comments