Na Victor Bariety;
UtanguliziMitihani ya kumaliza elimu ya msingi (PSLE) ni tukio muhimu katika mfumo wa elimu wa Tanzania. Kila mwaka, wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali wanakusanyika majukwaa haya ya elimu kupima maarifa na ujuzi walioupata. Mitihani hii siyo tu kipimo cha ufanisi wa mwanafunzi, bali pia ni kielelezo cha jitihada za taifa katika kuboresha na kuendeleza sekta ya elimu.
Takwimu za Mitihani ya Mwaka 2024 na 2023
Kwa mujibu wa NECTA:
Mwaka 2024, jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 1,172,279, wavulana 535,138 (45.65%) na wasichana 637,141 (54.35%).Watahiniwa waliochagua Kiswahili walikuwa 93.35%, na 6.65% walifanya mtihani kwa Kiingereza.
Watahiniwa wenye mahitaji maalum walikuwa 4,679, ikiwemo:
Wasioona: 92
Wenye uoni hafifu: 1,551
Wenye uziwi: 1,079
Wenye ulemavu wa akili: 448
Wenye ulemavu wa viungo: 1,509
Mwaka 2023, jumla ya watahiniwa walishiriki mtihani huu ilikuwa 1,397,293, ikionyesha kupungua kidogo mwaka 2024. Hata hivyo, idadi ya watahiniwa wenye mahitaji maalum imeongezeka, ikionesha jitihada za serikali kuhakikisha ushiriki wa watoto wote.
Ufaulu wa Watahiniwa
2023: 1,092,960 walifaulu (80.58%)
2024: 974,229 walifaulu (80.87%)
Wavulana waliifaulu: 507,920 (2023)
Wasichana waliifaulu: 585,040 (2023)
Chanzo: NECTA PSLE 2023 Report, NECTA PSLE 2024 Bulletin (necta.go.tz)
Takwimu hizi zinaonyesha msururu wa maendeleo endelevu, pamoja na jitihada za serikali kuhakikisha kila mwanafunzi anashiriki na kufaulu bila kizuizi.
Maandalizi na Utekelezaji wa Mitihani
NECTA imejizatiti kuhakikisha maandalizi ya mitihani yanafanyika kwa ufanisi. Miongoni mwa maandalizi haya ni:
Usambazaji wa karatasi za mtihani kwa wakati
Mafunzo kwa wasimamizi wa mitihani
Uhakikisho wa usalama wa vituo vyote vya mtihani
Huduma maalum kwa watahiniwa wenye mahitaji maalum
Kwa mwaka 2024, maandalizi yote yamekamilika ipasavyo, ikionyesha uwajibikaji mkubwa wa Baraza la Mitihani, shule, na jamii.
Umuhimu wa Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi
Mitihani hii ni muhimu kwa sababu:
Inatoa mwanga juu ya kiwango cha elimu kilichopatikana na wanafunzi
Inatoa fursa ya tathmini ya mfumo mzima wa elimu
Ni kigezo muhimu katika mchakato wa usajili wa wanafunzi katika shule za sekondari
Kwa njia hii, mitihani ya kumaliza elimu ya msingi inachangia maendeleo ya taifa siyo tu kama tukio la siku moja, bali kama mwongozo wa Taifa na mwanga wa matumaini kwa vizazi vijavyo.
Changamoto na Mapendekezo
Licha ya mafanikio yaliyopatikana, bado kuna changamoto zinazohitaji kushughulikiwa:
Upungufu wa vifaa vya kufundishia
Uhaba wa walimu wenye ufanisi
Changamoto za kiufundi katika mchakato wa usahili
Mapendekezo:
Kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu
Kutoa mafunzo endelevu kwa walimu
Kuboresha miundombinu ya shule
Hitimisho
Mitihani ya kumaliza elimu ya msingi ni tuzo ya Taifa yenye thamani isiyopimika, ikionesha jitihada za serikali, shule, na jamii katika kuhakikisha mafanikio ya wanafunzi na maendeleo ya taifa. Ni muhimu jamii na serikali kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu ili mitihani hii ibaki kielelezo cha maendeleo endelevu kwa watoto na Taifa kwa ujumla.
Mwisho
Imeandaliwa na Victor Bariety – 0757-856284
0 Comments