Na mwandishi wetu;
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka mkoa wa
Geita, Evarist Gervas, amewataka wananchi wa Kata ya Kamena kukipa kura nyingi
CCM katika uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa sera na ahadi za chama hicho ni za
kweli na zinatekelezwa.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata hiyo, Gervas amesema kuwa CCM ni chama pekee chenye dira ya maendeleo inayoonekana na inayotekelezwa kwa vitendo kote nchini.
“Ilani ya CCM inatekelezeka. Vyama vingine havieleweki hata wanatoa ahadi gani. Tuchague chama kinachotekeleza, si cha ahadi zisizoeleweka,” amesema Gervas huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Aidha, amewahimiza wakazi wa Kamena kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 29, ili kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kuongoza kwa kishindo na kuleta maendeleo ya kweli kwa wana Kamena.


0 Comments