TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MWENGE KUKAGUA MIRADI YA BILIONI 164/= MKOANI GEITA

Na Editha Edward;

MWENGE wa Uhuru, umewasili mkoani Geita, ukitokea Mkoa wa Mwanza na utakagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya shilingi bil. 164.

Mwenge wa Uhuru, umepokelewa katika viwanja vya Shule ya Msingi Rwezera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ukitokea jijini Mwanza.

Baada ya kupokea mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella, amesema Mwenge wa Uhuru, utakagua jumla ya miradi 61 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 164 , likiwa ni ongezeko kubwa, ikilinganishwa na mwaka jana ambapo miradi 65 yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 32, ilikaguliwa.

"Mwaka huu, mwenge utakimbizwa umbali wa kilometa 653, utakagua miradi mikubwa yenye thamani ya zaidi ya bilioni 164. 

"Hii ni ishara kwamba, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anaendelea kufanya kazi kubwa ya maendeleo katika Mkoa wa Geita," amesema Shigella.

Shigella, amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba.

Komba amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, utakagua, kutembelea na kuzindua miradi tisa ya thamani ya sh. bilioni 2.8.

 





Post a Comment

0 Comments