Na mwandishi wetu;
Mgombea udiwani wa Kata ya Bukoli, Faraji Rajabu Seif, amemshauri mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda kupitia tiketi ya CCM Dkt. Jafari, kuhakikisha anazingatia changamoto za wananchi iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge.Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Bugogo Senta, Faraji amemhimiza Dkt.Jafari kuwa kiongozi wa karibu na wananchi na asiwe mbunge wa kukaa mjini Dodoma tu bila kushughulikia matatizo ya wananchi waliomchagua.
“Wananchi hawa unaowaona
wanahitaji kuwa karibu na wewe, hivyo jitahidi katika uongozi wako uwe karibu
na wananchi wako,” amesema Faraji leo Oktoba 4 alipokua akiwahutubia wananchi.
Aidha, Faraji amesisitiza kuwa wananchi wa Jimbo la Busanda wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji kiongozi makini na mwenye kujitolea kuwa karibu na jamii ili kuzitatua.




0 Comments