Na Victor Bariety, Geita;
(Takwimu
zimerejewa kutoka hotuba ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nyang’hwale, Hussein Amar
Kassu, aliyekuwa akisoma kutoka kitabu cha Ilani ya CCM 2020–2025.)
Wakati mwingine, maendeleo hayahitaji kelele yanahitaji ushahidi.Na leo, ushahidi huo una jina moja: Nyang’hwale.Wapo waliodhani Nyang’hwale itabaki kuwa hadithi ya nyuma ya dunia kijiji cha vumbi, mashimo ya dhahabu, na matumaini yaliyokufa.
Leo,
historia imebadilika.
Nyang’hwale
imevaa suruali ya maendeleo, imevaa viatu vya kazi, na imeinua uso wake mbele
ya Tanzania nzima kwa kusema:
“TULITOKA MBALI, TUMEFIKA MBALI ZAIDI, NA TUNAENDA MBALI KULIKO WOTE.”
Miaka mitano tu nyuma, kulikuwa na sekondari 11 pekee katika jimbo lote.
Watoto
walitembea zaidi ya kilomita kumi kufika shuleni.
Zahanati
15 ndizo zilikuwa tegemeo la wananchi zaidi ya laki moja.
Maji
yalikuwa neema ya msimu.
Umeme
ulikuwa ndoto ya mbali.
Na mama
mjamzito alikuwa akihesabu hatima yake kwa moyo wa hofu, maana hospitali ya
wilaya haikuwepo.
Barabara zilikuwa majeraha ya udongo; magari yakizama, wagonjwa wakikosa msaada, na ndoto zikisalia majina tu kwenye kampeni.
2025: NYANG’HWALE INAINUKA KAMA ASUBUHI YA TUMAINI
Kati ya vumbi na jua kali, sasa inasimama Nyang’hwale mpya inayotembea kwa miguu ya maendeleo na kupumua kwa mapafu ya matumaini.
Kati ya mwaka 2020 na 2025, kwa mujibu wa Mbunge Hussein Amar Kassu, akirejea takwimu za Ilani ya CCM:
Sekondari zimeongezeka kutoka 11 hadi 20.
Shule za msingi kutoka 67 hadi 74.
Madarasa kutoka 715 hadi 1,003.
Nyumba za walimu zimeongezeka kutoka 370 hadi 389.
Maabara zimepanda kutoka 21 hadi 41.
Mabweni kutoka 4 hadi 10.
Elimu bure imegharimiwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 19.
Huko Kakola, chuo cha VETA kimejengwa — kielelezo cha uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuwapa vijana silaha ya maarifa badala ya maneno.
Mwandishi wa makala hii alikutana na Lydia Kisinza, mkazi wa Nyijundu, machozi yakimlenga:
“Tulikuwa tunaamka alfajiri, watoto wanatembea mbali. Leo shule ipo karibu, walimu wako, maji yapo, umeme unawaka. Mungu ambariki Mama Samia na CCM.”
AFYA
YANYWA HEWA YA UHAI
Zamani, mama mjamzito alipoumwa, safari yake ya kwenda kujifungua ilikuwa vita.
Leo,
Nyang’hwale ina hospitali ya wilaya mpya kabisa.
Zahanati
zimeongezeka kutoka 15 hadi 35, na vituo vya afya sasa ni 4.
Kwa mara
ya kwanza, kituo cha afya Busolwa kimepewa zaidi ya shilingi milioni 250
kukamilisha ujenzi.
Upatikanaji wa dawa umeongezeka kutoka asilimia 75 hadi 85, na vifo vya kina mama wakati wa kujifungua vimepungua kutoka 12 hadi 9 kati ya 100.
Hii ni
kwa sababu sasa huduma zipo karibu, barabara zinapitika, na maisha yamepata
thamani.
Kama anavyosema Mbunge Hussein Amar Kassu:
“Huu ni ushahidi wa kazi, si propaganda. Tumeacha historia ya maumivu, sasa tunaandika historia ya matokeo.”
MAJI,
UMEME NA BARABARA: NGUVU YA KAZI, MIZIZI YA MAISHA
Maji safi yameongezeka kutoka asilimia 39 hadi 77 bomba kila kijiji, tenki kila kata.
Serikali
inalenga kufikisha maji kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.
Vijiji 62 tayari vinawaka umeme, wachimbaji 114 wa madini wameunganishiwa umeme, mashine zinawashwa mchana na usiku.
Barabara
zinazopita kwa urahisi zimeongezeka kutoka kilomita 105 hadi 355, makaravati
kutoka 222 hadi 495, na taa za barabarani zimeshika mji wa Kharumwa usiku
kucha.
Kwa miaka mitano ijayo, ilani imeelekeza:
Barabara ya Kahama-Nyang’hwale-Busisi (Mwanza) kujengwa kwa kiwango cha lami.
Barabara za Kharumwa–Kakola na Nyaruguguna–Geita nazo kuwa lami.
Barabara za ndani za vijiji kufungwa kwa changarawe kilomita 288.
Haya yote ni matokeo ya kazi, si bahati.
SAUTI ZA WANANCHI: “HATUJENGI MANENO, TUNAJENGA MAENDELEO”
Jumane Sabuni, mchimbaji mdogo wa dhahabu, anasema kwa sauti yenye nguvu:
“Tukiandamana tutapoteza amani. Tukiweka tiki tunapata maendeleo. Maandamano hayaleti umeme, hayajengi shule. CCM imetuonyesha njia, kazi yetu ni kutiki.”
Kauli hiyo imekuwa wimbo wa Nyang’wale.
Watu
hawasubiri kuambiwa wanajua. Wameona kwa macho yao, wameshika kwa mikono yao,
wamehisi kwa maisha yao.
MUSSA MWAKITINYA: “AMANI NI MBONI YA MACHO YETU”
Mgeni rasmi wa mkutano, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Ndugu Mussa Mwakitinya, aliwasha moto wa uzalendo:
“Chungeni amani kama mboni za macho yenu. Amani ndiyo mama wa maendeleo. Tukitiki CCM, tunatiki kazi, tunatiki elimu, tunatiki afya, tunatiki taifa lenye heshima.”
HUSSEIN
AMAR KASSU: NGUVU YA KAZI, SAUTI YA WENYE MAENDELEO
Kwa muda wote wa miaka mitano, jina la Hussein Amar Kassu limekuwa alama ya msukumo wa maendeleo.
Anaposema
“nilimsumbua Rais Samia kwa maendeleo ya Nyang’hwale,” watu wanacheka kwa furaha kwa sababu anasema kweli.
Kila
alichodai kimefanyika: shule, barabara, zahanati, chuo, na umeme.
anasema
Kassu kwa sauti ya matumaini.
Ni alama
ya uthubutu wa viongozi na uamuzi wa wananchi waliosema:
Na kazi imefanyika.
Shule
zinacheka, hospitali zinapumua, maji yanatiririka, umeme unawaka, barabara
zinapitika, na mioyo ya watu imejaa matumaini.
Nyang’wale imekuwa kioo cha maendeleo ya vijijini nchini — kielelezo cha Tanzania inayotembea kwa miguu ya kazi na moyo wa umoja.
Maandamano? Hapana.
Hapa kazi
inaendelea na tiki ndiyo silaha ya maendeleo.
Imeandikwa na:
Victor
Bariety – Geita
Simu: 0757
856 284
PICHA ZAIDI












0 Comments