Na mwandishi wetu;
Mgombea Udiwani wa Kata ya Nyarugusu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samata Shabani Makula, amewaahidi wananchi na wanachama wa CCM kuwa ataiinua kata hiyo kimaendeleo endapo watamchagua kwa kura nyingi katika uchaguzi wa Oktoba 29.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Nyarugusu Senta, Samata amesema kuwa dhamira yake ni kuibadilisha Nyarugusu na kuifanya kuwa kata ya mfano kwa maendeleo ya kweli, hususan kwenye miundombinu ya barabara na huduma za kijamii.
Ametoa wito kwa wakazi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kumpa kura ili aweze kutimiza azma yake ya kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Nyarugusu.

0 Comments