Mkuu wa mkoa wa
Geita Mhandis Robert Gabriel amewataka wafanyabiashara wa saruji mkoani Geita
kuacha tabia ya kupandisha bei ya bidhaa hiyo kwani kwakufanya hivyo nikwenda
kinyume na matakwa ya serikali.
Akiwa katika
oparesheni ya kukagua bei ya saruji katika maduka ya vifaa vya ujenzi kwa
wafanyabiashara wa halmashauri ya mji wa Geita Novemba 23,2020 Mhandis Robert amebaini uwepo wa
ongezeko la bei ya saruji kutoka 19,500 hadi 22,000 bei ambayo imekuwa
kandamizi kwa wananchi wenye vipato vidogo.
Mhandis Robert
amewataka wafanyabiashara hao kuuza bidhaa
hiyo chini ya shilingi elfu 20 na kwa yeyote atakae kiuka agizo hilo
atachukuliwa hatua.
Akiwa katika oparesheni hiyo Kaimu meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita Bw Peter Njau ametumia nafasi hiyo kuwataka wafanyabiashara wote mkoani hapa kuacha tabia ya kujiamulia kuongeza bei za vifaa vya ujenzi nakuwakumbusha kuendelea kutoa risiti pindi wanapo uza na kununua bidhaa.
Mmoja wa
wafanyabiashara wa saruji katika mji wa Geita Bw Pius Magunja amekiri kuuza
saruji mfuko mmoja kwa bei ya shilingi elfu 22,000 nakuahidi kuachana na bei
hiyo nakuuza bei inayotakiwa.
Hivi karibuni akizungumza kwa njia ya video na wakuu wa mikoa wote hapa nchini WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) aliwaagiza kufanya ukaguzi kwenye viwanda vya kuzalisha saruji, mawakala, wauzaji wa kati na wadogo wa bidhaa hiyo na wachukue hatua stahiki.
0 Comments