Na Beatus Bihigi - Mtwara.
Bi. Rehema Athuman Malindi ambaye ni Katibu wa UWT wilaya ya Tandahimba ameamsha ari kwa wanawake wa kata ya Mndumbwe kuelekea zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwa kuwataka wajitokeze kwa wingi bila kuogopa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi serikali za mitaa.
" Nimekuja kuwapa ujasiri msiogope kuchukua fomu za kugombea" alisema Malindi.
Pamoja na mambo mengine aliyozungumzia mesisitiza umoja miongoni mwawanawake akiwaomba wapendane na kama kunamakosa wasameheane ili kuzidi kuimarisha umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Tandahimba.
Bi. Rehema Athuman Malindi (Katibu wa UWT wilaya Tandahimba) akiwahamasisha UWT kata ya Mndumbwe kupendana na kuendelea kuwa wamoja alipokuwa kwenye ziara yake leo 13 Mei 2024 |
Katika hali ya kuwaunganisha wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliohudhuria katika mkutano huo amewakumbusha wanawake wasisahau majukumu yao katika ndoa, wawasaidie waume zao shughuli zote ili kudumisha amani na upendo katika ndoa.
" Nisisikie ndoa imeharibika ati katibu amesema tukagombee, hapana" alisema Katibu wa UWT wilaya ya Tandahimba Bi. Malindi.
Amewasisitiza wanawake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuwahimiza vijana waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea washiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Katibu huyo wa CCM UWT wilaya ya Tandahimba katika ziara yake aliambatana na Mwenykiti wa UWT wilaya ya Tandahimba Mhe Bi. Alafa Twalib Nakatanda, Kisura Salum Namgugu (Mjumbe kamati ya utekelezaji wilaya ya Tandahimba), Asha Yusufu Nampondo (Mjumbe halmashauri kuu CCM wilaya),Somoe Sadick Chivalamba (Mjumbe kamati ya utekelezaji wilaya), Upendo Shaibu Mahundu (Mjumbe kamati ya utekelezaji wilaya) na Sofia Hamisi Chilidu (Mjumbe kamati ya utekelezaji wilaya ya Tandahimba).
Katika picha katikati ya wajumbe kamati ya utekelezaji wilaya ni Fatuma S. Mkavilima (Katibu UWT kata ya Mdimba) aliefika kwa mwaliko kumsikiliza Katibu UWT wilaya Tandahimba akiwa kata ya Mndumbwe. |
Mwisho
0 Comments