|
Mhe. W. B Mwanjelile -Hakimu mfawidhi mahakama ya mwanzo Namikupa akiwa katika shule ya sekondari Mndumbwe akitoa Elimu ya sheria ya mirathi. |
|
Mkuu wa Shule ya sekondari Mndumbwe katika Wilaya ya Tandahimba Mwl. Ntarisa K. Ntarisa (aliyesimama) na upande wa kulia kwake ni Mwl. Merick Mayala Nguna (Mwalimu wa somo la fizikia shuleni hapo), akipongeza na kuishukuru timu ya wanasheria kwa kufika kutoa Elimu ya sheria kwa Wanafunzi sheleni hapo leo 26 Januari 2024. |
Na mwandishi wetu - Mtwara.
Mkuu wa Shule ya sekondari Mndumbwe halmashauri ya Wilaya Tandahimba Mwl. Ntarisa K. Ntarisa amewapongeza mahakama ya Wilaya Tandahimba kufuatia ujio wa timu ya wanasheria na wasimamizi wa sheria kutembelea shule ya sekondari Mndumbwe kwa lengo la kutoa Elimu ya sheria kwa Wanafunzi katika wiki ya sheria ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu 2024 ni "Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa;Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai"
Mwl. Ntarisa ambaye ndiye Mkuu wa Shule ameishukuru serikali kwa kuona kuwa kunaumuhimu kwa Wanafunzi shuleni kupata Elimu ya masuala ya sheria ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbali mbali katika jamii, huku akiomba Elimu hii itolewe mara kwa mara mashuleni na kwenye jamii "Ningeomba wiki ya sheria walau iwemara mbili au mara tatu kwa kila mwaka na isiwe mara moja tu" alisema Mkuu wa Shule Mwl.Ntarisa.
|
Katika picha katikati ni Ntarisa K. Ntarisa (Mkuu wa Shule ya sekondari Mndumbwe), kushoto kwake ni Mhe. Bankunda J. Bitwale (Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo Mahuta) na upande wa kulia ni Mwl. Merick Mayala Nguna, Mwalimu wa somo la fizikia shuleni hapo. |
|
Baadhi ya Wanafunzi katika shule ya sekondari Mndumbwe Wilayani Tandahimba wakimsikiliza mtoa mada katika wiki ya sheria Moses Clement Ndullumba ambaye ni mwendesha mashitaka katika Mahakama ya Wilaya Tandahimba (aliyesimama). |
|
Aliyesimama ni Mhe. W. B. Mwanjelile Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo Namikupa akiwasilisha mada kuhusu mirathi katika shule ya sekondari Mndumbwe leo 26 Januari 2024. |
|
Mhe. Bankunda J. Bitwale (Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo Mahuta) akitoa Elimu kwa Wanafunzi wa Shule ya sekondari Mndumbwe juu ya sheria ya mtoto, na kushoto kwake ni Moses Clement Ndullumba ambaye ni mwendesha mashitaka katika Mahakama ya Wilaya Tandahimba |
|
Mkaguzi msaidizi wa jeshi la Polisi na Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Mambamba (A/Insp.) Kasike D. M akitoa mada wakati wa wiki ya sheria katika shule ya sekondari Mndumbwe akiwahimiza Wanafunzi kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria akitaka wazingatie masomo. |
Mwisho.
0 Comments