TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

KANISA LA ANGLIKANA LAJITOSA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO NCHINI

Mhashamu Baba Askofu Wa Kanisa La Anglikana Jimbo La Victoria Nyanza Zephania Amos Ntuza akitoa ujumbe kwa waumini wake baada ya kumaliza ibada ya kipaimara kanisa la kristo mfalume lililopo geita mjini.


NA SALUM MAIGE,GEITA. 

Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza limeanza kutoa elimu kwa waumini wake kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watoto na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili kutokomeza vitendo hivyo kwa watoto na kutunza nguvu kazi ya Taifa la baadaye.

Hatua ya Kanisa hilo inakuja kufuatia kuibuka kwa vitendo vingi vya kikatili dhidi ya watoto ikiwemo ubakaji,ulawiti na mauaji ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika maeneo mbalimbali hapa nchi na kuleta hofu kwa jamii hasa yenye hofu ya Mungu.

Mhashamu baba Askofu wa Kanisa hilo Kanda ya Victoria Nyanza Zephania Amos Ntunza amesema hayo wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi muda mfupi baada ya Ibada ya Kipaimara kwa watoto iliyofanyika kwenye kanisa la Anglikana la Kristo Mfalme lililopo mjini Geita.

Mhashamu Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Victoria Nyanza Zephania Amos Ntuza Akitoa Kipaimara Kwa Watoto wa Kanisa la Anglikana la Kristo Mfalume lililopo Geita mjini.

Amefafanua kuwa,Viongozi wa kanisa Hilo wameanza kutoa elimu kwa waumini wao kupinga ukatili hilo pamoja na kuwataka waumini kutoa taarifa za ukatili unaofanyika kwenye jamii dhidi ya watoto ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.

Sisi viongozi wa dini tumeamua kutofumbia macho vitendo  hivi vya kikatili dhidi ya watoto,kwani vinaumiza sana ,sisi tunaposikia watoto wanachomwa mikono,wanabakwa,wanapigwa,na wengine wanauawa kikatili tunasikitika sana na sisi hatuwezi kukaa kimya”anasema Askofu huyo.

Ameongeza kuwa kanisa linaendelea kuiombea nchi ili waharifu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kikatili waweze kuacha mara moja na wanaendelea kuwapa elimu waumini kutofumbia macho matukio hayo badala yake wajitokeze kwenda kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Aidha,Mchungaji wa Kanisa la Kristo Mfalume Anglikana mjini Geita,Joseph Samwel Kitwe amesema,hatua ya askofu huyo kuwaelekeza kuanza kuwaelimisha waumini wao juu kupinga ukatili hatua nzuri na kwamba wao kama viongozi wa dini watahakikisha wanafikisha ujumbe huo kwa waumini wao.

Anasema,Katika Vitendo vya Kikatili kwenye Mkoa wa Geita ni vingi na vinaleta hofu kubwa kwa jamii na kwamba kutoa elimu kwa waumini kujitokeza kutoa taarifa kwa vyombo vya dola itasaidia sana kuokoa watoto wengi ambao wengi wao wamekuwa wakiathirika na matukio hayo ya kikatili.

Tumepokea ujumbe wa baba askofu kuendelea kukemea vitendo vya ukatili katikati ya watoto na wamama,hili ni suala tunaendelea kulifanyia kazi”anasema Mchungaji Kitwe.

Nao baadhi ya waumini wa kanisa hilo Joyce Seka na James Mtalitinya wamesema matukio hayo ya kikatili yanatokana na watu kukosa hofu ya Mungu na kwamba ili kuthibiti matukio hayo njia pekee ni kuhakikisha kila mmoja anabeba ujumbe wa baba Asfoku wa kutoa taarifa za matukio hayo.

Mmoja wa Watoto waumini wa Kanisa Hilo Amos Jacob amesema watoto kwa sasa hawana amani ndani ya nchi yao hasa matukio ya kikatili yanavyozidi kujitokeza na kusikika kwenye masikio yao.

Tunamshukuru baba Askofu kwa Kutambua haya matukio na kwa kauli yake inaonyesha yanamuumiza sana ,na sisi tunaomba wazazi,walezi wetu watulinde…na pia wajitahidi kuwapeleka watoto makanisani kusali…hawa wanaofanya ukatili dhidi yetu inaonyesha hawana hofu ya Kumuogopa Mungu hata Kidogo”anasema Amos.

Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Saphia Jongo ameunga mkono hatua ya Kanisa hilo ya kutoa elimu kwa waumini,huku akisema jeshi la polisi litaanza kupita kwa wananchi kuwapa elimu ya kupinga ukatili.

Geita kuna vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ,kilichopo ni kutoa elimu kwa wazazi na walezi ili kuwapa watoto wao malezi bora..Chanzo cha ukatili ni wazazi kutowapa malezi bora ..badala yake watoto wanakuja kuwa na usugu na inapotokea hapo wazazi wanakuwa na hasila wanawaadhibu vibaya na kusababisha wengine vifo”anasema RPC.

Anaongeza kwa kusema kuwa,watoto hawalelewi katika Hofu ya Mungu ili kuepukana na matukio hayo ni kurudi kwa jamii kuwapa elimu na kuwaelimisha kuwa kwa imani yao kila mmoja anatakiwa kuwajibika katika malezi yaliyo bora.

Mhashamu Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Victoria Nyanza Zephania Amos Ntuza Akitoa Kipaimara Kwa Watoto wa Kanisa la Anglikana la Kristo Mfalume lililopo Geita mjini.

Ripoti ya jeshi la polisi nchini Tanzania inaonesha ongezeko la asilimia 25.95 la ukatili dhidi ya watoto. Katika mwaka 2020 visa 7,388 viliripotiwa kote nchini tofauti na mwaka 2015 ambapo matukio 5,803 yaliripotiwa.

Watetezi wa masuala ya haki za watoto wametaja imani za kishirikiana na utandawazi kuwa miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa matukio hayo.

Ripoti ya hii ya jeshi la Polisi nchini inakuja katika kipindi hiki ambacho wazazi na walezi wengi wanatajwa kutokuwa karibu na watoto wao,wengi wakijihusisha na kusaka maisha bora ili kukidhi mahitaji ya msingi ya watoto huku wakiwapora haki ya kuwasikiliza.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments