|
Katikati ya hifadhi ya msitu wa Geita, shughuli za kilimo zikiendelea kuharibu mazingira. |
Mgalu ameongeza kuwa katika kuhakikisha mbinu mbadala zinatumika kurejesha hali ya uoto wa asili na kukabiliana na uharibifu huo ofisi yake imelazimika kuualika uongozi wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Geita,Taasisi na makundi mbalimbali kwenye kilele hicho ili kwenda kutoa
elimu kwa jamii, na makundi mbalimbali na kuhamasisha jamii kukabiliana na kasi ya uharibifu wa Hifadhi za Misitu .
“Hifadhi ya Misitu imegawanyika katika majimbo matatu ya uchaguzi jimbo la Geita Vijijini linalowakilishwa na mwanasiasa machachari Joseph Kasheku Msukuma, jimbo la Busanda na jimbo la Geita Mjini lina wakilishwa na Mbunge Constantine John
Kanyasu aliyewahi kuwa Naibu waziri wa Malia sili na Utalii na akiwa naibu waziari wa maliasili liachangia
kupunguza kasi ya uharibifu huo kwa kutoa elimu’’ anasema Meneja Mgalu .
|
Picha ya kuonesha hali ilivyo katika hifadhi ya msitu wa Geita ulivyo athiriwa na shughuli za kilimo holela. |
Meneja huyo alifafanua kuwa katika jimbo la Busanda linalowakilishwa na Mbunge Tumiani Magesa hifadhi ya Lwamgasa imeharibiwa sana kutokana na ufugaji, kiliomo, uchomaji mkaa, huku shughuli za uchimbaji wa Madini zikiwa
kinara kwa uharibifu wa mazingira ya hifadhi za Misitu .
“Kwa Mbunge Constantine John Kanyasu alipokua Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii alitumia fusra hiyo kuwashawishi wananchi wa mkoa wa Geita kupunguza kasi ya uharibifu wa hifadhi za Misitu na kuwapatia elimu wakazi na Wananchi wa maeneo yaliyopakana na hifadhi za Misitu na hivyo kupunguza
kasi iliyokuwepo .
Pia Mbunge Kanyasu alitumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wapiga kura wake na kuwajengea utamaduni wa kulinda hifadhi kwa kuigeuza Hifadhi ya Misitu kuwa fursa katika uwekezaji kwa kushawishi vijana na wazee kuanzisha vikundi ambavyo
vilianzisha miradi ya ufugaji nyuki na baadhi ya wananchi kugeuka kuwa
walinzi wahiyo Misitu .
|
Meneja TFS Geita Bw. Almas Hamis Mgalu akiwa katika kuhamasisha zoezi la kupanda miti katika mipaka ya hifadhi ya msitu wa Geita (Demarcation).
Hata hivyo meneja huyo hakusita kuzitaja baadhi ya changamoto zinazo ikabiri idara hiyo kuwa ni pamoja na upungufu wa watumishi katika idara hiyo hali inayosababisha kushindwa kukabiliana na kasi ya wimbi la uharibifu huo ambao unafanywa mara nyingi kwa kuwahusisha makundi tofauti wakiwemo watu wanaoishi jirani ya hifadhi ya Misitu hiyo.
Naye Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Geita Robert Nyamaigoro aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo anakiri kuwepo kwa uharibifu wa hifadhi za misitu, hivyo zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na suala la uhifadhi wa mazingira siyo la hiari wala lelemama isipokuwa ni lazima. | Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Geita Robert Nyamaigoro akipanda mti |
Ambapo alisema kuwa wakati juhudi za serikali ya chama hicho CCM zinaendelea kuhakikisha mji wa Geita unakuwa wa kijani kama hapo awali. Uharibifu wa mazingira unaathari kubwa kama vile kusababisha ukame,mabadiliko ya tabia nchi na kupotea kwa baadhi ya viumbe hai na wanyama.
Aidha zoezi la uwekaji wa mipaka katika maeneo ya hifadhi (Demarcation) limekuja siku chache kufuatia agizo la waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt. Angelina Mabula alilolitoa kwa wakala wa misitu alipotembelea mkoani Geita na kukutana na wadau wa ardhi wakiwemo wabunge, madiwani na viongozi wa |
chama na serikali mkoani hapa katika ukumbi wa GEDECO mjini Geita.
Akiwa mkoani Geita Dkt. Mabula aliagiza wakala wa misitu TFS kuweka mipaka katika maeneo ya hifadhi kutenganisha makazi ya wananchi ili kuondoa migogoro na wananchi, “TFS wekeni mipaka yenu itambulike kuondoa migogoro,nilifika hapa Geita nikiwa mwenyekiti wa timu ya mawaziri nane”.
Mbunge Kanyasu katika maombi yake kwa Waziri wa Ardhi alidai kuwa Msitu wa hifadhi wa Usindakwe ulikuwa umepoteza sifa ya kuendelea kuwa hifadhi na
hivyo waziri Mabula na kamati yake aliombwa kuchukua hatua za makusudi kumaliza kilio hicho cha muda mrefu cha wakazi wa Halmashauri ya mji wa
Geita na hifadhi ya Msitu wa Usindagwe itolewe kwa matumizi ya kibinadamu akidai kuwa hifadhi ya Msitu huo imepoteza sifa aliomba Mbunge Kanyasu .
|
Gari la TFS Geita likiwa na miche ya miti katika zoezi la kupanda miti kuonesha mipaka ya hifadhi ya msitu wa Geita (Demarcation). |
Kilio hicho cha wananachi wa Geita kupitia Mbunge Kanyasu kikamgusa waziri Dkt. Mabula hatua iliyoplekea kuongozana na wawakilishi wa TFS hadi katika eneo la hifadhi hiyo na kujionea hali ilivyo ambapo waziri Mabula akahitimisha mjadala wa kilio hicho cha Wananchi wa Mji wa Geita kwa kuahidi jambo hilo
kulifanyia kazi akishirikina na wizara ya maliasili na Utalii .
Mbunge wajimbo la Bukombe Dkt. Doto Mashaka Biteko ambae pia ni waziri wa Madini katika kikao cha waziri Mabula naye aliomba kuangaliwa kwa jicho la huruma kwa maeneo ya hifadhi za misitu yaliyopoteza sifa katika jimbo lake
ili yaweze kutolewa kwaajili ya shughuli za binadamu za kilimo na ufugaji hali ya uhitaji huo inatokana na uwepo wa ongezeko la kasi la idadi ya watu.
Mwisho.
0 Comments