Na Alphonce Kabilondo,Geita
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu Geita Gold Mine (GGML) imetoa msaada wa vifaa 8 vya kuhifadhia taka kwa wafanyabiashara wa soko la Nyankumbu Mtaa wa uwanja halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani hapa .
Mhandisi wa mazingira Mgodi wa GGML Josephine Kimambo akitoa elimu ya usafi wa mazingira wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo amesema kuwa usafi wa mazingira ni muhimu .
Alisema kuwa uchafuzi wa mazngira kwenye soko hilo usipodhibitiwa unaweza kusababisha kuibuka magonjwa ya mulipuko ikiwemo kuhara pamoja na kipindupindu hivyo jambo la usafi wa mazingira ni mwarobaini pekee .
Enos Mareli ,Mwenyeki wa mtaa wa uwanja (alievaa gloves kulia) akipokea vifaa vya kuhifadhi taka taka kutoka mgodi wa dhahabu GGML. |
Kimambo alisema kuwa mgodi huo umekuwa ukitoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa jamii kwa makundi tofauti ili kukabiliana na hali ya mabadiriko ya tabianchi .
“Mgodi wa GGML tutaendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na kusaidia jamii na kuhakikisha jamii ya geita inanufaika na uwepo mgodi wa GGML" alisema Kimambo.
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo Enos Mareli akipokea msaada wa vifaa hivyo ameupongeza uongozi wa mgodi wa GGML na kuahidi kuwa vifaa hivyo vitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Aliongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa taka kwenye masko mawili ya Mtaa soko la asubuhi Nyankumbu ,na soko la jioni ambapo ametumia fursa hiyo kuziomba kampuni zingine wadau pamoja na taasisi kuiga mfano wa mgodi huo wa kusaidia jamii .
“Tunaupongeza mgodi wa GGML kwa msaada huu vifaa tulivyo vipokea leo baadhi vitabaki soko la asubuhi nyankubu kifaa kimoja kitapelekwa ofisi ya Mtaa wa Uwanja lengo ni kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwenye masoko hayo" alisema mwenyekiti Mareli .
Vifaa vilivyokabidhiwa na mgodi wa GGML kama vinavyoonekana katika picha , nyuma yake ni viongozi wa serikali ya na uongozi wa soko la Nyankumbu mjini Geita na Maafisa kutoka GGML. |
Aidha mwenyekiti wa soko hilo Mchele Mhangwa alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja muda mwafaka kabla ya kupata msaada huo walikuwa wakilazimika kufagia taka na kuzibeba kwa kutumia mifuko na kupeleka eneo kukusanyia taka na baadae kusombwa na gari.
Mwisho.
0 Comments