Na
Samwel Masunzu;
Klabu
ya waandishi wa habari mkoa wa Geita (GPC) imesema itaendelea kutimiza wajibu
wa kuhabarisha umma na kushiriki huduma za kiuchumi kupitia miradi ya kiuchumi
katika jamii
Hayo yamelezwa na katibu mtendaji msaidizi wa
klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Geita Ernest Magashi wakati wa makabidhiano ya pikipiki tatu ambazo
zimenunuliwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo la geita
Magashi
alisema waliomba kiasi cha shilingi million kumi kutoka Ofisi ya Mbunge wa
jimbo la Geita Mjini kupitia mfuko wa jimbo, na amekiri kuwa GPC ilipokea kiasi
cha shilingi millioni saba na laki tano, fedha ambayo kamati tendaji ya GPC
iliridhia zinunuliwe pikipiki tatu aina ya SanLG zenye thamani ya shilingi
milioni sita na laki tisa.
“Tuliomba
million kumi kutoka Ofisi ya Mbunge kwaajili ya ununuzi wa pikipiki moja na
guta, lakini tulipokea kiasi cha shilingi milioni saba na laki tano ambapo
kamati tendaji iliridhia kununua pikipiki tatu badala ya pikipiki moja na guta,
na hii ni kutokana na fedha kutokutosheleza kununua pikipiki moja na guta moja
kama ilivyokuwa imekusudiwa”Alieleza Magashi
Awali
kabla ya kukabidhi pikipiki hizo, Mbunge wa jimbo la Geita mjini Costantine
Kanyasu amesema hatua hiyo ni kuunga mkono waandishi wa habari kwa kutambua
nafasi yao katika jamii.
“Vyombo
vya habari ni muhimili wa nne nchini kati ya mihimili mine nchini ambayo ni
serikali kuu, mahakama na bunge, hivyo kukosekana kwa waandishi wa habari ni sawa
na kukosa jicho”
Aidha alisema pikipiki hizo zitasaidia kuwafikia wananchi wa vijijini na kuibua kero zao kwa haraka.
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari mkoni Geita Renatus Masuguliko alishukuru ofisi
ya Mbunge kwa kutambua mchango wa vyombo vya habari hasa zilivyopo ndani ya
GPC, na kueleza kuwa pikipiki hizo zitasaidia katika kurahisisha shughuli za
kiutendaji na kujikwamua kiuchumi na kutokuwa tegemezi.
Hata
hivyo baadhi ya wadau wa habari mkoani Geita Ivan Bwoya na Costantine Kalala wamesema
katika kuelekea uchaguzi mkuu wanaamini waandishi wa habari ni chachu ya kutoa
elimu katika kuwajengea uelewa wananchi.
0 Comments