 |
Amina Lada Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya sekondari Mndumbwe wilayani Tandahimba mkoani Mtwara. |
Na. Beatus Bihigi - Mtwara
Shule ya sekondari Mndumbwe ni shule ya kutwa ya wavulana na wasichana iliyopo katika wilaya Tandahimba mkoani Mtwara nchini Tanzania, ambayo inasimamiwa na Mwalimu Ntarisa K. Ntarisa ambaye ndiye Mkuu wa Shule hiyo.
 |
Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe Ntarisa K. Ntarisa (aliyevaa suti) alifurahi pamoja na Wanafunzi wake wakati wa burudani ya muziki kwenye sherehe ya Welcome Form One shuleni hapo leo 20/02/2025. |
Katika kuhakikisha taaluma ya Wanafunzi inaboreka, shule hiyo imekuwa ikiandaa sherehe maalum ya kuwakaribisha Wanafunzi wanaokuwa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo maarufu kama "Welcome Form One".
 |
Madam Mwansite W. Shali, Mwalimu wa michezo na burudani Mndumbwe sekondari akisherehesha siku ya kuwakaribisha kidato cha kwanza 2025. |
Kufuatia hatua hiyo, Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya kuwakaribisha kidato cha kwanza alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo ambapo amewakilishwa vyema na Makamu Mwenyekiti wa Bodi Bi. Amina Lada ambaye pamoja na mambo mengine amesema Wanafunzi wengi wanashindwa kufanya vizuri sana katika masomo kutokana na maadili yao kuwa siyo mazuri.
 |
Pichani ni MC nambari moja na mtaalamu wa somo la kiswahili shuleni hapo Mwalimu Faraji Athuman (aliyevaa shati ya bluu) na Benedict Mnali (mwenye kofia nyeusi) wakiserebuka na Wanafunzi wakati wa sherehe. |
"Wazazi tukae na watoto wetu, watoto wa kike wamebweteka na maisha maisha ambayo hawajapata maisha na watoto wa kiume nao wamekuwa siyo watu wakushaurika,tukae nao nyumbani tuongee nao tuwasaidie suala la maadili tusiwaachie walimu tu" alisema Bi. Lada.
 |
Amina Lada Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya sekondari Mndumbwe wilayani Tandahimba mkoani Mtwara. |
Mzee Maulidi Mshamu Askari mstaafu wa jeshi la wananchi wa Tanzania alipata fursa ya kutoa nasaha kwa kidato cha kwanza na Wanafunzi wote kuwa wazingatie elimu " Shikilia elimu, Elimu ndio mkombozi wa maisha yenu" alisema Mzee Mshamu.
 |
Mzee Maulidi Mshamu (Maarufu kama Mjeshi - mwenye microphone) Askari mstaafu wa jeshi la wananchi wa Tanzania na mdau wa Elimu Tandahimba mkoani Mtwara |
Amesema kuwa enzi zao shule zilikuwa chache sana ila kwa wakati huu serikali chini ya Mhe. Rais Dokta Samia Suluhu Hassan ameboreha Elimu kwa kujenga majengo ya kisasa madarasa ya kutosha maabara na nyumba za walimu, hivyo amewataka wasome kwa bidii.
 |
Kulia ni Afisa mifugo Bi. Mtukacha na kushoto ni Mwalimu Juma Said Dadi wakitoka kumpa zawadi (kumfupa) mwanafunzi mwenye kipaji cha kucheza aliyetamba na kibao cha Disconnect (akionekana kwa nyuma yao) |
Nae Isabella Blasio Katibu wa UWT CCM kata ya Mndumbwe wakati alipopata nafasi ya kutoa neno kwa kidato cha kwanza na Wanafunzi wote amewasisitiza kusoma kwa bidii na kuepuka vitendo viovu na tabia ya utoro. Pia amewaomba walimu kuendelea kujitoa kuwasaidia Wanafunzi na kuwapa haki yao ya Elimu ili wafikie ndoto zao.
 |
Isabella Blasio ambaye ni Katibu wa UWT CCM kata ya Mndumbwe akipokea kipaza sauti kutoka kwa MC Faraji.
|
Pia Benedict Mnali ambae ni Askari wa jeshi la Polisi mstaafu amewataka Wanafunzi kuwa na nidhamu nzuri ili waweze kufaulu masomo yao na kuwa vile wanavyotaka kuwa maishani.
 |
Benedict Mnali Askari mstaafu wa jeshi la Polisi na mdau wa Elimu akitoa neno kwa Wanafunzi hususan wakidato cha kwanza shuleni hapo leo 20 Februari, 2025
|
Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Mndumbwe mzee Naheru Saidi akiwanasihi Wanafunzi wa shule ya sekondari Mndumbwe wakati wa sherehe ya kuwakaribisha kidato cha kwanza amesema kuwa anawapongeza walimu wa shule ya sekondari Mndumbwe kwa juhudi wanazofanya kuhakikisha Wanafunzi wanafaulu masomo.
 |
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mndumbwe mzee Naheru Saidi akitoa neno katika sherehe ya kuwakaribisha kidato cha kwanza Mndumbwe sekondari 2025. |
Amesisitiza kuwa Elimu ndio kila kitu hata kilimo, biashara, na hata kupanda kurosho inahitajika Elimu.
 |
Shaban Hassan Nampwahi mwakilishi wa vijana katika sherehe hiyo akiwaasa Wanafunzi kuzingatia masomo bila kujali changamoto zitakazo jitokeza. |
 |
Wazazi, walimu na wageni waalikwa wakipata chakula cha pamoja |
 |
MC na moja ya wadau wa Elimu pamoja na Wanafunzi wakiburudika |
 |
Shaban Nampwahi akiwa katika furaha wakati wa sherehe kuwakaribisha kidato cha kwanza Mndumbwe sekondari Tandahimba Mtwara. |
 |
Baadhi ya wazazi waliohudhuria sherehe ya Welcome Form One Mndumbwe sekondari leo tarehe 20/2/2025 |
 |
Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakimpongeza na kumuaga Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe Ntarisa K. Ntarisa (katikati) |
 |
Mkuu wa shule Mndumbwe sekondari Ntarisa K. Ntarisa (aliyevaa koti) kulia kwake ni Mwalimu wa taaluma shuleni hapo Mathayo Kwaslema (aliyeandika nne) na kushoto kwake ni Mwalimu wa fedha Christopher Matiko na wamwisho ni kiranja wa stoo Twaifu wakifurahi wakati wa muziki Maarufu kama Dimbe. |
Mwisho.
0 Comments